Search images and videos on Instagram. Most Popular Hashtags and Users.Stalist
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea photos and videos on Instagram

Medias attached with hashtag: #itaendelea on Instagram

lifestyles and history (@simulizi_tz) Instagram Profile Photosimulizi_tz

lifestyles and history

 image by lifestyles and history (@simulizi_tz) with caption : "Part 5
Niliyanunua na akaanza kuyatumia. Aliyatumia kwa muda lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote. Salim alianza kuwa mw" - 1958766230785734115
ReportShareDownload419

Part 5 Niliyanunua na akaanza kuyatumia. Aliyatumia kwa muda lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote. Salim alianza kuwa mweusi tii usoni na ngozi yake ilikuwa ikibabuka kama chura mzee. Nilijipa matumaini labda ngozi yake inapona taratibu na kubadilika ili iweze kurudi katika rangi yake ya awali ya maji ya kunde. Niliyanunua na akaanza kuyatumia. Aliyatumia kwa muda lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote. Salim alianza kuwa mweusi tii usoni na ngozi yake ilikuwa ikibabuka kama chura mzee. Nilijipa matumaini labda ngozi yake inapona taratibu na kubadilika ili iweze kurudi katika rangi yake ya awali ya maji ya kunde. Je salim atapona ugonjwa wake wa ngozi au ndio watampoteza kabisa! Usikose kuendelea nasi katika story hii ambayo imehusisha maisha ya kweli ya mtanzania mwenzetu kupitia hapa hapa @simulizi_tz #itaendelea

lifestyles and history (@simulizi_tz) Instagram Profile Photosimulizi_tz

lifestyles and history

 image by lifestyles and history (@simulizi_tz) with caption : "Mambo 39  yanayovunja mahusiano ya kimapenzi au ndoa.
1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mpenzi au mwenzi wako! 
Ku" - 1956507235920330648
ReportShareDownload011

Mambo 39 yanayovunja mahusiano ya kimapenzi au ndoa. 1. Kutokuwa na mawasiliano ya karibu na mpenzi au mwenzi wako! Kumbuka mawasioiano ya karibu ni kila kitu hasa mwenye mapenzi. Kuna kitu hukipendi? Amekukasirisha? Au kuna kitu umekisikia kikizungumzwa? Jitahidi kupata ukweli kutoka kwake na jitahidi kukiamini huku ukifuatilia kwa makini ukweli wake. Hapa nasisitiza mawasiliano ni kila kitu katika maisha ya mapenzi. 2. Kutokujali maumivu ya mwenzi au mpenzi wako. Kumbuka unapoishi na mtu au kukubali kuwa nae katika mahusiano ya mapenzi au ndoa, wewe ni mfariji wake wa kwanza pale anapopatwa na jambo lolote baya au la kuhuzunisha. Wewe ni mtu ambaye unaweza ukamvuja au kumjenga na vilevile una nguvu ya kumfanya asimame hata kama anapitia gumu kiasi gani. Hivyo itumie nafasi yako vyema kwa kuwa nae karibu sana na kumfariji hasa kipindi anapopitia mitihani flani flani ya maisha. 3. Ubishi usiokuwa na maana! Jitahidi kuwa mtu wa kukubali makosa yako na kukubali kujifunza kutokana na makosa yaliyotendeka. Sio kila kitu kibaya au ugomvi unapotokea baina yenu unakuwa mtu wa kumlaumu mwenzio na kumfanya ajione kama hana thamani tena na nimkosaji. Jitahidi kujishusha hasa pale unapoona kuwa ni kweli umekosea. 4. Kupenda kujihesabia haki. Watu wa namna hii Mara nyingi wanapenda sana kukosoa makosa ya wenzi wao lakini inapotokea yeye amekosea hataki hata asemeshwe au aulizwe. Kama uko kwenye mahusiano na binadamu wa namna hii jua kwamba Upo na mtu mbinafsi sana na anajiangalia yeye tuu. Hawa ndo wale watu ambao haruhusu uwe na marafiki au hataki kuona ndugu zako nyumbani kwenu ila ndugu zake hawaoni kama tatizo kwake. 5. Kutokubali kosa. Binadamu wa namna hii ni ngumu sana kuishi nae na anajiona ni binadamu aliekamilika na kila baya linapotokea anaona wewe ndo kisababishi. Mfano kwa wanaume hawa ndo wale ambao ikitokewa mimba kwenye uhusiano wenu atasema ulimtegeshea au ulipata kwa makusudi yako mwenyewe! Kama Upo na mtu wa namna hii jibebe na ujipange. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "Hadithi:MREMBO LATIFA 09
MTUNZI: EDO MAN “Nitajiua tu,” alijisemea Nahra na kujibanza sehemu huku akisubiria treni ipiti" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955344677890146325

Hadithi:MREMBO LATIFA 09 MTUNZI: EDO MAN “Nitajiua tu,” alijisemea Nahra na kujibanza sehemu huku akisubiria treni ipitie na yeye kulala relini. Aliyachoka maisha yake hiyo ndiyo sababu iliyompelekea kutaka kujiua siku hiyo. Hakutaka kuendelea kuishi na wakati watu wote aliokuwa amewaamini hawakutaka kuishi na yeye. Moyo wake ulimuuma, hakukuwa na kitu kingine alichokiona kuwa suluhisho la maisha yake zaidi ya kujiua tu. Alidhamiria kufanya hivyo kwa kuamini kwamba asingeweza kuumizwa tena, asingeweza kulia tena, huko atakapokuwa, angeishi maisha matamu milele na kuepuka ghadhabu za dunia hii. “Pooooooo,” ilisikika honi ya treni ya mizigo, alipoisikia honi hiyo, akachungulia kwa jicho moja kutoka pale ukutani alipojibanza. Treni ile ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi. Ilikuwa imetoka kituoni na kuanza safari yake, alipoiona treni hiyo kwa mbali, Nahra akasubiri mpaka ikaribie na ndiyo aende kujilaza relini na hatimaye aweze kufa na kuyaepuka mateso aliyokuwa akiyapata. “Nisamehe Mungu! Mateso yamezidi, acha tu nijiue ili wazazi wangu wapumzike, wasinichukie tena. Pia nisamehe kwa kukiua hiki kiumbe unachokitengeneza tumboni mwangu. Mungu, sifanyi hivi kwa kupenda, najua unayajua maisha ninayopitia,” alisema Nahra huku treni ile ikiendelea kusogea zaidi. Nahra aliendelea kuisubiria,treni ilibakisha kama hatua mia mbili kabla ya kufika pale alipotaka kujilaza. Kichwa chake kilitawaliwa na mawazo tele, alikuwa tayari kujiua lakini si kuendea kuishi kwa mateso kama aliyokuwa akiishi. “Bora nife tu, sina haja ya kuendelea kuishi,” alisema Nahra. Baada ya sekunde kadhaa, treni ilikuwa mbali kama hatua mia moja, alichokifanya Nahra, akakimbilia relini na kujilaza. Machozi yalimbubujika mashavuni mwake, hakuamini kama maisha yake yote aliyokuwa akiishi, mwisho wa siku alikuwa amefikia hatua ya kujiua. “Nisamehe Mungu, sikupenda kujiua, ila sina jinsi. Acha nife na mwanangu aliyepo tumboni,” alisema Nahra, treni ya mizigo ilikuwa ikija kwa kasi, na ilibakisha hatua arobaini tu za miguu ya binadamu kabla ya kumkanyaga pale relini alipokuwa amelala. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:MREMBO LATIFA 08
MTUNZI: EDO MAN “Nikusaidie nini?” aliuliza Mithun huku akijitahidi kujizuia kupumua kupitia pu" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955091042170031543

HADITHI:MREMBO LATIFA 08 MTUNZI: EDO MAN “Nikusaidie nini?” aliuliza Mithun huku akijitahidi kujizuia kupumua kupitia pua yake, maji yaliyokuwa yameilowanisha nguo ya Nahra, yalikuwa yakinuka. “Naomba unisamehe,” alisema Nahra huku akijitahidi kupiga magoti chini. Alikuwa akilia kwa maumivu makali, alijua kwamba alifanya makosa kumkataa mwanaume huyo aliyekuwa na lengo la kumuoa na kumkubali Deo aliyekuwa amemfukuza kama mbwa. Macho yake yalionyesha kila kitu, alikuwa akiomba msamaha lakini Mithun hakujali. Alikumbuka vema kila kitu kilichotokea katika maisha yake ya nyuma na binti huyo. Alimpenda Nahra na kuahidi kumuoa lakini maamuzi ya msichana huyo yalikuwa kwa Deo, mwanaume mweusi aliyempa mimba na kumtimua. “Unanuka Nahra,” alisema Mithun maneno yaliyomuumiza mno Nahra, ila kwa kuwa alikuwa na uhitaji, akavumilia. “Naomba unisamehe Mithun.” “Nikusamehe ili iweje? Na hicho kitumbo ukipeleke wapi? Nikusamehe wewe? Ulivyonikataa kwa maneno ya dhihaka! Nahisi umepotea njia. Kwanza unanuka sana, hivi ulioga jana?” alisema Mithun na kuuliza kwa dharau. Kilio cha Nahra kikaongezeka zaidi, hakuamini kama maneno yale yote yalitoka Mithun. Alijitahidi kuomba msamaha lakini matokeo yale aliambulia maneno ya kejeli tu, hakutaka kuendelea kubaki mahali hapo, akaondoka zake huku akilia. “Nitakwenda wapi mimi? Nitaishi vipi mimi? Bora nikajiue tu, siwezi kuendelea kuishi,” alijisemea Nahra na huku akipiga hatua kuelekea nje ya ghorofa hilo. Huo ndiyo ulikuwa uamuzi alioufikia, hakutaka kuendelea kuishi tena, mateso na maumivu aliyoyapitia yalitosha kabisa kumfunza, hivyo alitaka kujiua kwa kuamini kwamba angekwenda kupumzika. Akaanza kukimbia kuelekea Kariakoo Relini huku lengo lake kubwa ni kwenda Mivinjeni. Hakukuwa na kitu alichokifikiria zaidi ya kujiua tu, alitaka kuiondoa roho yake kwa kulala kwenye reli na treni kupita juu yake. Mara baada ya kufika Kariakoo Relini, akachukua Barabara ya Kilwa na kunyoosha nayo kama alikuwa akienda Bandarini. Alipofika Mivinjeni, akaanza kuelekea katika reli iliyokuwa chini ya daraja ambako kulikuwa na vyumba vingi vya reli ya kati. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 07
Mtunzi: EDO MAN “Nitamtafuta tu,” alisema Deo huku akijipa uhakika kwamba angeweza kumuona ten" at Dar es Salaam, Tanzania - 1955087855195237036

HADITHI: MREMBO LATIFA 07 Mtunzi: EDO MAN “Nitamtafuta tu,” alisema Deo huku akijipa uhakika kwamba angeweza kumuona tena Nahra aliyekuwa na mimba yake. **** Nahra alikuja kupata fahamu asubuhi, alikuwa katika majani yenye unyevuunyevu, mwili wake ulikuwa ukimuwasha. Pamoja na kuwashwa huko, alikuwa akisikia maumivu makali chini ya kitovu. Akaanza kujiuliza sababu ya yeye kuwa mahali hapo, hakukumbuka kitu chochote kile, alibaki akishangaa mpaka kumbukumbu zilipokaa sawa na kuanza kukumbuka kila kitu kilichotokea usiku uliopita, Nahra akaanza kulia, akajiangalia, sehemu zake za siri zilikuwa zimeharibiwa vibaya, akaendelea kulia mfululizo huku akijiinua kuelekea barabarani. Kila mtu alibaki akimshangaa, alionekana msichana mrembo mno lakini muonekano wake ulikuwa tofauti kabisa, alikuwa msichana mchafu mno, kwa jinsi uzuri wake ulivyokuwa, hakutakiwa kuwa kama alivyokuwa. “Hata kama nimechafuka na hata kama nimebakwa, bado ninahitaji kumuona Mithun, ni lazima nimfuate na anisaidie, sina kimbilio jingine zaidi yake,” alisema Nahra. Kila alipopita, watu walimshangaa, hakuwa akitembea kawaida, alikuwa akichechemea kama mtu aliyekanyaga mwiba. Alitembea hivyohivyo mpaka alipofika maeneo ya Fire ambapo akaunganisha mpaka Mtaa wa Twiga, mtaa uliokuwa na maghorofa mengi, huko ndipo alipokuwa akiishi Mithun. “Mungu, naomba Mithun anikubalie, anisamehe kwa kila kitu niweze kuwa naye, asahau kila kitu kilichotokea maishani mwetu,” alisema Nahra, tayari alikuwa amefika katika mlango wa nyumba ya kina Mithun, akaanza kugonga mlango, moyo wake ulijawa hofu. Wala hazikupita dakika nyingi, mlango ukafunguliwa, mtu aliyekuwa akimuhitaji ndiye aliyefungua mlango, alikuwa Mithun. Mwanaume huyo alibaki akimwangalia Nahra huku uso wake ukiwa kwenye mshangao mkubwa. Hakuamini kama yule aliyesimama mbele yake alikuwa Nahra yule aliyekuwa akimfahamu au alikuwa mtu mwingine. Alikuwa mchafu mno, nguo zake zilikusanya majanimajani huku zikiwa zimetapakaa tope, kwa kumwangalia tu, Mithun alijisikia kinyaa. “Nikusaidie nini?” aliuliza Mithun huku akijitahidi kujizuia kupumua kupitia pua yake, maji yaliyokuwa yameilowanisha nguo ya Nahra, yalikuwa yakinuka. #ITAENDELEA

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI: MREMBO LATIFA 06

Wazazi wa Nahra walionekana kuwa tatizo kwake. Mara baada ya kumpa mimba msichana huyo na kuh" at Dar es Salaam, Tanzania - 1954362415010791129

HADITHI: MREMBO LATIFA 06 Wazazi wa Nahra walionekana kuwa tatizo kwake. Mara baada ya kumpa mimba msichana huyo na kuhamia kwake kwa kuwa wazazi wake walimfukuza, wazazi hao wakawatuma wanaume wawili waliokuwa na bunduki, walichokuwa wakikitaka ni kuona Deo akimfukuza Nahra nyumbani hapo, vinginevyo, wangemuua. Huo ulikuwa mtihani mkubwa maishani mwake, alimpenda Nahra, hakutaka apate tabu yoyote ile, kitendo cha kuambiwa amfukuze msichana huyo kilikuwa kigumu, akakataa. Watu hao walipoona kwamba kitu hicho hakikufanyika, wakarudi kwa mara ya pili, wakati huu walionekana kuwa na hasira zaidi, kila walipomwangalia Deo usoni, waliyakumbuka maneno ya mzee Patel ambaye aliwaambia wamuue tu. “Kijana, fanya tunachokwambia. Tumeagizwa tuje kukuua, hatuwezi, tunakuonea huruma. Fanya hivyo, tunakupa siku moja ya ziada, kesho tukija, tunakuja na sura tofauti na hizi,” alisema mwanaume mmoja huku akimwangalia Deo usoni. Kwa jinsi walivyoonekana, kwa maneno yao yaliyowatoka midomoni mwao ilionyesha kabisa watu hao walimaanisha kile walichokiongea, Deo akakubaliana nao kishingo upande. Siku hiyo usiku ndiyo ilikuwa siku ya kumfukuza Nahra nyumbani hapo. Alifanya hivyo huku moyo ukimuuma mno, kila alipomwangalia msichana huyo, alijisikia huruma, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali. “Nahra, naomba unisamehe, sikutaka kukufukuza, wazazi wako ndiyo waliolazimisha kufanya hivi, ninakupenda Nahra,” alisema Deo huku akimuona Nahra akikimbia, machozi yalikuwa yakimmbubujika msichana huyo, baada ya hapo, hakujua Nahra alikimbilia wapi, usiku huo, kwake ukawa usiku wenye mateso mengi. #ITAENDELEA.

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "HADITHI:HAL AND HANS ( PENZI LA MISUKOSUKO) 31
MTUNZI:HB
.  Ilikua ni saa kumi na moja na nusu wakati anaoga ..simu ilii" at Dar es Salaam, Tanzania - 1950760137481753296

HADITHI:HAL AND HANS ( PENZI LA MISUKOSUKO) 31 MTUNZI:HB . Ilikua ni saa kumi na moja na nusu wakati anaoga ..simu iliitana ilkua ni simu ya mama yake inamuomba afike nyumbani ili akameleke hosp...Huyo ilikua ni mwalimu Ahmed akiwa nyumbani kwake pekeake kwa mke wake aliku a kijijini kwa ajili ya kujifungua..mama yake mwalimu Ahmed alikua ni mgonjwa wa pressure ya kupanda ...mida anampigia simu mwanawe ili afike ilikua pressure imepanda..aliwasha gari lake na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mama yake. kwa yeye ilikua anaishi mji mwengine..alipofika njiani aliombwa msaada na Halima na kuamua kumsaidia na ndio yakampata hayo yalio mpata..hivyo ndio ilivyo kua.. Hospitali wakati Halima anapatiwa matibabu na kwavile hawakutaka kumsikiliza Halima alichukua mkasi kwa nguvu na kutishia kujiua.. Naomba nyote muondoke au la sio hivyo nitajichoma mkasi wa tumbo nife..na wala asijaribu mtu kunizuia nitajiuaa.nipisheni mlangoni...ilikua ni sauti ya Halima kwani aliamua kutumia nguvu ili akamsaidie mwalimu Ahmed. ........Ilikua ni katika msitu mmoja ambao ilikua kama nimakaazi ya Bi Aisha kulikua na kambi moja kubwa ya majangili huko ndio aliko pelekwa Hassan. Nabahat nzuri wakati anashushwa katika gari Hassan tayari fahamu zilisha mjia na anafahamu kila kitu kinacho endelea ..alichukuliwa na kuingizwa katika chumba kimoja kizuri sana chumba hicho nia alichokua akiishi bi Aisha humo.aliingizwa na chumba kikakomewa kwa mnje ..baada ya muda mfupi tu bi Aisha aliingia huku akiwa na kanga moja.. Karibu nyumbani kwangu mume wangu hapa ndio tutakapo ishi katika maisha yako yote .. Aliketi katika kitanda huku Hassan akiwa amekaa chini akiwa na mawazo chungu mzima...njoo hapa kitandani basi mpz mbona unanikasidikia hivyo.. Aliinuka kitandani na kuamua kumsogelea hapo ili ambembeleze Hassan.Hassan hakufanya tabu alikubali kunyanyuka na alikubali kuelekea kitandani kwani hakua na jinsi..bi Aisha alikuwa ni mwingi wa story huku akijifanya ni mwema sanaa mbele ya Hassan..kibaya zaid Alimdanya Hassan eti ilkua katekwa na Halima na yeye ndio kamkomboa...alizani Hassan alikua hana kumbukumbu lakini kumbe hassan alikua na kumbukumbu zake zote #itaendelea